>SERIKALI ya Tanzania imewakaribisha wawekezaji katika kuongeza thamani ya mnyororo wa bidhaa za kilimo, ufugaji na uvuvi na kusema mazingira ya uwekezaji ni rafiki.
Akizungumza katika kuitangaza Tanzania na vivutio vyake katika Jukwaa la kilimo biashara lililoandaliwa na taasisi ya Jukwaa la Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRF), na kufanyika Kigali Rwanda kwa njia ya video, Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba alisema Tanzania ipo tayari kwa uwekezaji.
Alisema pamoja na kuwezesha mazingira rafiki, kuwa kisiwa cha amani,Serikali ya Tanzania imetengeneza miundombinu ambayo inawezesha wawekezaji kufikia soko la ndani na nje.

Comments
Post a Comment