>Taasisi ya Kiota Woman Heath and Development (KIWOHEDE) imewajengea uwezo waandishi wa habari vijana (young reporter) juu ya kuandika habari zinazohusiana na haki za binadamu.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mwanasheria wa kujitegemea Bright Msalya, ambapo kwa fursa hiyo amewasihi waandishi wa habari kuzijua na kuzifahamu haki za binadamu ili waweze kuandika habari zinazohusiana na haki za binadamu.
Aidha waandishi wa habari vijana (YOUNG REPOTERS) wamekumbushwa namna ya kuibua na kupaza sauti juu ya habari zinahusu uvunjifun wa masuala ya haki za bianadamu.
Mafunzo hayo ya haki za binadamu yanaratibiwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya KIWOHEDE kwa kushirikiana na dlab,TADIO, TIB,UTPC kwa hisani ya Shirika la We world.

Comments
Post a Comment