>Marekani inatekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa wa kike kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70, kulingana na Wizara ya Sheria.
Lisa Montgomery alimnyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata mama huyo tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba mwaka 2004.
Anatarajiwa kuchomwa au kudungwa sindano ya sumu Desemba 8.
Mwanamke wa mwisho kuhukumiwa kifo na serikali ya Marekani alikuwa Bonnie Heady, aliyekufariki dunia kwenye chumba cha gesi huko Missouri mwaka 1953, kulingana na kituo cha taarifa za adhabu ya kifo.
.
#drixnews

Comments
Post a Comment