NEC; MPIGA KURA ANAWEZA KUOMBA KARATASI NYINGINE AKIKOSEA AU KUBADILI UAMUZI

 

>Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefafanua utaratibu huo ikisema, Mpiga kura aliyeharibu karatasi kwa bahati mbaya anaweza kuirudisha kwa Msimamizi wa Kituo na kuomba nyingine ili apige kura vizuri

Ofisa wa NEC, Flora Mkama amesema, "Inawezekana wapiga kura hawajui kuwa wana Haki ya kuomba karatasi nyingine ya kupigia kura endapo itatokea kwa bahati mbaya amekosea au amebadili uamuzi wake"

Amefafanua, "Inawezekana mtu amekosea katika kuchagua akakuta ameweka alama kwa Mgombea ambaye hakumtaka au ameamua kubadilisha uamuzi, kuliko aharibu ile karatasi kwa kukatakata anatakiwa airudishe kwa Msimamizi alafu aombe nyingine akapige"

Aidha, ametoa wito kwa Wapiga kura kufuata maelekezo ya Msimamizi wa Kituo na kuepuka kukiuka taratibu za Uchaguzi ili kuepusha migogoro

.

#drixnews

Comments