> Bobi Wine aliwasili kwenye kituo cha uteuzi akiwa ameandamana na mke wake.
.
Sasa ni rasmi kuwa Bobi Wine atakabiliana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu mwaka ujao mwaka 2021.
.
Baada ya stakabadhi zake kukaguliwa, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Justice Simon Byabakama alisema “Tumethibitisha stakabadhi zilizowasilishwa na mgombea kwamba ametimiza vigezo vyote vya uteuzi.”
.
Bobi Wine pia alikumbushwa kwamba mikusanyiko ya umma bado imepigwa marufuku na kwamba kampeni zake zote zitaendeshwa kulingana na miongozo ya Tume ya Uchaguzi.
.
#drixnews

Comments
Post a Comment