SERIKALI YATOA ELIMU JUU YA UNUNUAJI DAWA KWENYE MADUKA YA MADAWA


  Na Tatu Tambile.

SERIKALI imewataka wananchi kutonunua dawa katika maduka ya dawa pasipo kupata idhini ya cheti cha Daktari. 

Wito huo umetolewa leo Jijin Dar es salaam na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi wakati wa maadhimisho ya Wiki ya kuzuia Usugu wa Vimelea vya Maradhi ya Kuambukiza ambapo amesema kuwa watu wamekuwa wakinunua  dawa bila ya kufuata muongozo wa Daktari Jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao.

"Wananchi wasinunue wala wasitumie dawa bila ya kupata maelekezo kutoka kwa Daktari, pia 

wauzaji wa Maduka ya dawa wasiwauzie watu dawa ya binadamu au  ya mifugo bila ya Cheti kutoka kwa Daktari." Amesema

Profesa Makubi amesema kumekuwa na matumizi mabaya ya dawa za Antibiotiki ambapo Asimilia 50 ya dawa hizi zinatumiwa kwa matumuzi ya wanyama na binadamu kinyume na taratibu za kitabibu, Jambo ambalo ni hatari kiafya kwa binadamu na wanyama.

Comments