RC kunenge "wazazi wafanye maandalizi mapema kwa watoto"

 Na Tatu Tambile.

Mkuu wa Mkoa Abubakari M. Kunenge amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi waliomaliza elimu ya msingi kufanya maandalizi mapema ili matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha Kwanza yatakapotangazwa waweze kuwapeleka watoto wao kwenye shule walizopangiwa tarehe 11/01/2021 bila kukosa.

Haya ameyazungumza leo Jijin Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wakati akitoa taarifa ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya shule ya msingi mwaka 2020 katika Mkoa wa Dar es salaam.

Amesema ufaulu Mkoa wa Dar es salaam umepanda kutoka asilimia 93.26 ya mwaka 2019 hadi asilimia 93.50 kwa mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 0.24, ambapo Mkoa wa Dar es salaam umeshika nafasi ya Kwanza (01) Kitaifa Kati ya mikoa 2

Kunenge amesema matokeo hayo yameufanya Serikali kupitia Mkoa kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa halmashauri kujipanga kuwapokea wanafunzi wote waliofaulu ambapo jumla ya Tsh. 16,040,000,000 zimetengwa kwa ajili ya madarasa 802 na jumla ya Tsh. 2,604,128,000 pia zimetengwa kwa ajili ya kuandaa samani zitakazotumiwa na wanafunzi hao ambazo ni viti na meza 38,296.

Kunenge anashukuru Serikali ya awamu ya tano kwa jitihada inazozifanya kwa kuhakikisha mpango wa upatikanaji wa elimu ya msingi bila malipo unatekelezwa kama ilivyokusudiwa, pia Maafisa elimu, walimu, wajumbe na kamati za shule na wadau mbalimbali pamoja na wazazi na walezi kwa ufatiliaji mzuri wa watoto wao.



Comments