Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka waajiri kuwaajiri walemavu katika Sekta mbalimbali kwasababu wana uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Hayo ameyazungumza leo Jijin Dar es salaam katika maadhimisho ya miaka 60 ya Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) amesema waajiri watakiwa kuwapokea na kuwapa ushirikiano walemavu waweze kupata fursa ili kuchochea maendeleo na kupata kipato ili kujikwamua kiuchumi.
Waziri Mkuu mesema watu wenye ulemavu wapo wenye elimu na uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika Sekta mbalimbali.
hivyo amesema waajiri waweke kipaumbele watu wenye ulemavu kama ambavyo Serikali inavyotekeleza kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kupata nafasi mbalimbali za uongozi.
Hata hivyo amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha waajiri wanawekewa mazingira wezeshi kwa waajiri kuweza kufika hatua nzuri ya uwekezaji ili kusaidia watu katika makundi mbalimbali ikiwemo watu wenye ulemavu, wanawake na Vijana kupata fursa ya ajira.

Comments
Post a Comment